Mungu Wa Ajabu

Mungu Wa Ajabu
André Cronje
Mungu wa Ajabu: Ni utukufu wa wafalme kutafuta siri za dunia na kupata siri za ufalme wa Mungu. Dunia yote imejaa utukufu wake, na viumbe vyote vinapaaza sauti vikitaja jina lake kwa sifa na kuabudu. Mungu wa Ajabu imejaa mashairi na sifa ili kuhamasisha imani yako na mkusanyiko wa mawazo. Kama vile mtunga-zaburi alivyosema, ulimi wangu ni ule wa mwandishi aliye tayari kumpa ukuu mfalme wangu.


Mungu wa Ajabu
Mungu ni mkuu na wa kutisha. Jina lake ni la Ajabu.

André CRONJE
Translated by Winnie Ngimor
Hakimiliki
Ina leseni kwa ajili ya uboreshaji binafsi na inaweza kutumika kwa ujenzi wa maadili na kutia motisha. Hakuna sehemu inayoweza kunakiliwa tena kwa faida au kuuza tena.

André Cronje © 2020 Hakimiliki
Sanaa ya Dhana na André
Heshima maalumu kwa King James.
Mwandishi
Andre ni mzaliwa wa Afrika Kusini mzao wa Huguenot anayeishi Paris, Ufaransa. Yeye ni msanii, mwandishi, na mmiliki wa duka mtandaoni la nguo za Kikristo. Kama mfinyanzi aumbavyo udongo wake, ndivyo anavyounda na kuboresha mawazo yake kuhusu mada anuwai, kwa sanaa ya dhana, na fasihi ya kinabii, akisisitiza maswala ya kijamii, kimaadili, na kiroho na nuru ya Yesu Kristo, ambaye alikufa na kufufuka, akisamehe dhambi, akiponya wagonjwa, na ni mtoaji wa uzima wa milele, kwa yeyote anayeamini na kubatizwa kwa jina lake.
https://andrecronje.me (https://andrecronje.me/)
Yaliyomo
Hakimiliki
Mwandishi
1. Wimbo wa Yesu
2. Ni Siku Nzuri
3. Msifuni Yah
4. Yesu Rafiki Yangu
5. Hakuna Kisichowezekana
6. Imba na Uombe
7. Yeye ni Mkuu Zaidi
8. Mungu Baba
9. Niko Peke Yangu
10. Tatu, Mbili, Moja
11. Kuishi kwa Imani
12. Mlima Songa!
13. Tumaini Tena
Baraka Kwako
1. Wimbo wa Yesu
Yesu wewe Ndiye wangu, Yesu wewe Ndiye unayeangaza, Yesu wewe ni, Shujaa wa Pekee, aliyetoka mbinguni na kunitenga, kwa ajili ya ufalme wako na utukufu wako, Bwana.
Yesu wewe Ndiye wangu, jua kali, nuru ya ulimwengu, angazia maisha yangu, na uangaze kupitia mimi, nuru gizani, ili wote waweze kuona, kuwa wewe Ndiye, mwana wa Pekee wa Mungu .
Yesu wewe Ndiye wangu, neno la Mungu, Imanueli, Mungu pamoja nasi, mwana wa binadamu, mtoto wa bikira na mwana wa Baba, Aliyetumwa kutoka mbinguni na ujumbe kwa kila mtu, mnyenyekevu na mpole uliwafundisha watu wote, geuka kutoka kwa dhambi na umgeukie Mungu, ukweli umekuja, ambao utakuweka huru.
Yesu wewe Ndiye wangu, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa wote, juu ya mabega yako utawala wa sheria. Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Hakuna mungu mwingine, hakuna jina lingine, Mtu wa huzuni uliponya maumivu yangu, kutoka msalabani hadi kwenye kaburi tupu, ulifufuka tena, jahanamu imeshindwa, Kristo amefufuka, nimezaliwa mara ya pili.
Yesu wewe Ndiye wangu, rafiki wa rafiki yangu mwenye dhambi, uliponya wagonjwa, na kusamehe uhalifu, ukibadilisha maji kuwa divai. Viziwi watasikia, na bubu watazungumza, vipofu wataona watu wenye ukoma wakitakaswa, wafu wakitembea mara nyingine tena.
Yesu wewe Ndiye wangu, neno la Mungu lililotabiriwa, mwana-kondoo wa Mungu atatolewa kafara, simba wa Yuda mfalme wa Wayahudi, mwenye nguvu, wa ajabu, mshauri, mfalme wa amani, tangu milele hata milele, Baba, mimi ni mtoto wako,
Yesu wewe Ndiye wangu, Yesu wewe Ndiye unayeangaza, Yesu wewe ni, Shujaa wa Pekee, aliyetoka mbinguni na kunitenga, kwa ajili ya ufalme wako na utukufu wako, ndiyo mfalme wangu, - haleluya usifiwe Yesu.
2. Ni Siku Nzuri
Ni siku nzuri ya kuimba sifa zako, ni siku nzuri iliyojaa upendo na neema. Ni siku nzuri kukujua, Mungu, Ni siku nzuri dhambi zangu zimeoshwa. Ni jambo zuri kusifu na kuimba, ndiyo, kukutawaza Bwana na mfalme. Ni siku nzuri na njia tunayojua.
Ni siku nzuri, ndio maana nakuja mapema kuomba. Ni siku nzuri nitakaa pamoja na Mungu. Ni siku nzuri iliyojaa jua na mvua ya thamani. Ni siku nzuri nakupa upendo wangu. Ni siku nzuri iliyojaa zawadi kutoka juu. Ni siku nzuri, wewe ni sababu yangu maneno hayatoshi.
Ee Mungu wangu, ni siku nzuri, Ee Mungu wangu njia ni nzuri jinsi gani. Ee Mungu wangu pamoja nawe nitakaa, Mungu Wangu maneno hayatoshi.
Ni siku nzuri, Mungu wangu, na njia zako pia. Wewe ndiye sababu ya kutabasamu nikifanya mengi zaidi, na wewe ndiye sababu yangu kuimba. Mfalme wangu mpendwa, kwani nilipopata njia yako, nilipata nyumba yangu, Ee Mungu wangu pamoja nawe nitakaa. Ee Mungu wangu, ni siku nzuri. Nitakufuata kupitia njia iliyonyooka na nyembamba.
Ee Mungu wangu, ni siku nzuri. Ninapokea upendo wako, zawadi kutoka juu. Ee Mungu wangu, ni siku nzuri ya kujaa upendo, amani, na furaha. Ni siku nzuri, Mungu wangu, ni siku nzuri kwa sababu upo katika mwendo wote.
3. Msifuni Yah
Msifuni Yah, kwa mdundo, Msifuni Yah, kwa wimbo. Kwa sababu ya Yesu, siishi tena maisha ya uhalifu. Neema na rehema ipo kwenye mishipa yangu, ikiendeshwa na injili na jina lake.
Akiwa ametubu na kusamehewa, mzee huyo aliaga dunia, kila kitu ni kipya, nimezaliwa mara ya pili. Roho tembea juu ya mistari hii, pumua uhai na utuache tuangaze. Maneno ya imani, nyimbo za neema jinsi alivyopata aibu kama hiyo, msalaba wa aibu, haki ililemazwa lakini siku tatu baadaye Kristo akafufuka, sasa tumaini langu liliongezeka, zaidi ya kaburi hilo tupu.
Msifuni enyi watu wote, Msifuni malaika na viumbe vyote, Msifuni hekaluni, na msifuni kwenye kiti chake cha enzi. Msifuni sasa, wakubwa kwa wadogo Ndiyo, msifuni Yah, milele na milele.
4. Yesu Rafiki Yangu
Yesu, rafiki yangu, ukigeuza maji kuwa divai. Tafadhali njoo kwenye harusi yangu na sherehe yangu. Njoo na Roho wako wa uzima na maji ya uzima, kwani marafiki wangu pamoja na mimi, Bwana, tuna kiu. Leta furaha kwa nyumba zetu, marafiki na familia, unapomwaga divai yako bora mwishowe.
Yesu, rafiki yangu, ukigeuza maji kuwa divai, nyumba yako ya mawe yaliyo hai inapendeza jinsi gani. Tumejazwa na hazina na manukato ya mbinguni, tunasubiri sauti ya bwana harusi wetu. Kuvikwa taji na kuketi pamoja na Bwana wetu na kumsikia akisema: Njoo bi harusi wangu mpendwa, vyumba vyako viko tayari, karamu ianze. Njoo ule na unywe pamoja nami, katika nyumba ya baba yangu, divai na mkate ninao kwa ajili yako.
Ee Yesu, rafiki yangu, mwenye kusamehe na mwenye fadhili, jinsi ulivyogeuza maji yangu kuwa divai. Njooni sasa enyi watu wa kabila la dunia na visiwa, njooni mataifa, wadhaifu na wenye nguvu, mkate wa baraka wa mbinguni utatuliza laana ya dunia ya njaa. Hasira ilizuiliwa, na amani na Mungu kwa damu yake ya thamani. Yesu, rafiki yangu, jinsi gani umegeuza maji yangu kuwa divai.
5. Hakuna Kisichowezekana
Hakuna kilicho cha kina sana, Anaweza kukiruhusu
kielee.
Hakuna kitu cha kudumu, Hawezi kukibadilisha.
Hakuna kitu kisicho na tumaini, Anaweza
kukirejesha.
Hakuna kitu cha zamani sana, Anaweza kukifufua.
Hakuna kitu kinachoumiza sana, Anaweza
kukifariji.
Hakuna kitu kilichovunjika sana, Anaweza
kukirekebisha.
Hakuna kitu cha kutisha sana, Anaweza
kukifukuza.
Hakuna kitu ambacho hakiwezi kudhibitiwa,
Anaweza kukidhibiti.
Hakuna kitu kilicho mbali sana, Anaweza kukifikia.
Hakuna kitu duni sana, Anaweza kufanya
kifanikiwe.
Hakuna kitu kilichofichwa sana, Anaweza kukipata.
Hakuna kitu kigumu sana, Anaweza kukilegeza.
Hakuna kitu ambacho kinaugua sana, Anaweza
kukiponya.
Hakuna kitu kilichofungwa sana, Anaweza
kukifungua.
Hakuna kitu kitupu sana, Anaweza kukijaza.
Hakuna kitu kidhaifu sana, Anaweza kukiimarisha.
Hakuna kitu kidogo sana, Anaweza kukizidisha.
Hakuna kitu kisicho na maana sana, Anaweza
kukikuza.
Hakuna kitu kisichoeleweka sana, Anaweza kukifafanua.
Hakuna lisilowezekana kwa yeye anayeamini.
Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana,
Yeye atafanya.
6. Imba na Uombe
Hii ndiyo siku ambayo Bwana ameifanya
Nami nitafurahi na kushangilia ndani yake.
Nitaimba na kuomba,
bila kujali nini kinakuja kwangu.
Mimi nipo kila wakati na nimekamilika,
kwa upendo wake na neno lake.
Mimina ndani yangu utukufu wako,
mimina hadithi yako kutoka kwangu,
jinsi ulivyokufa na kufufuka,
hiyo ni furaha yangu na matumaini.
Na sifa moyoni mwangu,
na shukrani,
Ninaendesha mbio hii,
na kupaaza sauti neema ya kushangaza.
Nilipata nafasi yangu,
ambapo wakati sio raha,
Mbele yako ninaishi milele,
Haleluya, nitaimba na kuomba.

Конец ознакомительного фрагмента.
Текст предоставлен ООО «ЛитРес».
Прочитайте эту книгу целиком, купив полную легальную версию (https://www.litres.ru/pages/biblio_book/?art=63808576) на ЛитРес.
Безопасно оплатить книгу можно банковской картой Visa, MasterCard, Maestro, со счета мобильного телефона, с платежного терминала, в салоне МТС или Связной, через PayPal, WebMoney, Яндекс.Деньги, QIWI Кошелек, бонусными картами или другим удобным Вам способом.
Mungu Wa Ajabu André Cronje

André Cronje

Тип: электронная книга

Жанр: Стихи и поэзия

Язык: на языке суахили

Издательство: TEKTIME S.R.L.S. UNIPERSONALE

Дата публикации: 16.04.2024

Отзывы: Пока нет Добавить отзыв

О книге: Mungu wa Ajabu: Ni utukufu wa wafalme kutafuta siri za dunia na kupata siri za ufalme wa Mungu. Dunia yote imejaa utukufu wake, na viumbe vyote vinapaaza sauti vikitaja jina lake kwa sifa na kuabudu. Mungu wa Ajabu imejaa mashairi na sifa ili kuhamasisha imani yako na mkusanyiko wa mawazo. Kama vile mtunga-zaburi alivyosema, ulimi wangu ni ule wa mwandishi aliye tayari kumpa ukuu mfalme wangu.

  • Добавить отзыв